Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kibiashara ya Milimani afariki

Martin Mwanje
1 Min Read
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kibiashara ya Milimani  Zena Atetwe Rashid Jalenga

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kibiashara ya Milimani  Zena Atetwe Rashid Jalenga ameaga dunia. 

Jaji Mkuu Martha Koome anasema Hakimu Rashid alifariki dunia mapema leo asubuhi, Oktoba 20, 2024 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Katika taarifa, Jaji Koome amesema wakati wa kipindi chake cha kuhudumu, mwenda zake alifanya kazi kwa dhamira ya kuhakikisha kudumishwa kwa utawala wa sheria na haki kwa mujibu wa maadili ya katiba.

“Kwa niaba yangu na ile a idara ya mahakama, natuma risala za rambirambi kwa familia yake, marafiki na wapendwa wake,” alisema Jaji Koome katika salamu zake za rambirambi.

“Tunamwomba Mwenyezi Mungu atupe ujasiri wa kustahimili kipindi hiki kigumu na amlaze marehemu mahali pema poponi.”

 

Share This Article