Hafla ya mazishi ya Raila Amolo Odinga yaanza huko Bondo

Marion Bosire
1 Min Read
Mahakama yakataa kusimamisha mazishi ya Raila Odinga.

Hafla ya mazishi ya waziri mkuu wa zamani Raila Amolo Odinga imeanza katika uwanja wa chuo kikuu cha Jaramogi Oginga Odinga huko Bondo kaunti ya Siaya.

Shughuli hiyo imefunguliwa kwa ibada ambayo inaongozwa na kanisa la Kianglikana.

Mama Ida na wanawe waliwasili katika eneo hilo muda mfupi tu kabla ya kuanza kwa ibada wakiwa wameandamana na viongozi kadhaa akiwemo Spika wa Seneti Aamason Kingi, mwanabiashara Jimmy Wanjigi na wengine.

Raila aliaga dunia Oktoba 15, 2025, akiwa na umri wa miaka 80, akipokea matibabu nchini India. Mazishi yake yanaandaliwa leo siku chache tu baadaye kutokana na kile kilichotajwa kuwa matakwa yake kwamba azikwe katika muda wa saa 72.

Website |  + posts
Share This Article