Hafla ya kumuapisha Prof. Kindiki yaendelea KICC

Martin Mwanje
1 Min Read

Hafla ya kumuapisha Naibu Rais mteule Prof. Kithure Kindiki inaendelea kwa sasa katika Jumba la Mikutano ya Kimataifa la KICC. 

Prof. Kindiki amewasili katika jumba hilo tayari kula kiapo katika hafla itakayosimamiwa na Jaji Mkuu Martha Koome.

Rais William Ruto, Kinara wa Mawaziri Musalia Mudavadi, Maspika wa mabunge yote mawili Moses Wetang’ula (Bunge la Taifa) na Amason Kingi (Seneti), Magavana, wabunge, mawaziri na Wakenya kutoka matabaka mbalimbali ni miongoni wanaohudhuria hafla hiyo.

Tutakuteletea maelezo zaidi hivi punde. 

Share This Article