Habari kuhusu afya sasa zinatolewa kwa wakati, asema Dkt. Amoth

Alitaja utoaji huduma za afya ya jamii kwa njia ya dijitali, uboreshaji wa vituo vya afya na mfumo wa Bima ya Afya ya Jamii, kama sehemu ya mabadiliko hayo.

Tom Mathinji
1 Min Read
Dr. Patrick Amoth - Mkurugenzi Mkuu wa Afya nchini Kenya.

Mkurugenzi Mkuu wa Afya Dkt. Patrick Amoth, amesema mfumo wa afya nchini Kenya umeimarika, huku habari kuhusu afya sasa zikitolewa kwa wakati.

Kulingana na Dkt. Amoth maendeleo ya dijitali sasa yanafanikisha usambazaji wa habari kutoka mashinani hadi ngazi za kitaifa, na kuwawezesha watoaji maamuzi kuelewa hitaji lililopo na kuchukua hatua za haraka.

“Kwa miaka kadhaa, maamuzi kuhusu afya yalitegemea utafiti uliochukua muda mrefu. Kenya imechukua mkondo tofauti, habari kuhusu afya sasa zinatolewa kwa wakati,” alisema Dkt. Amoth.

Alitaja utoaji huduma za afya ya jamii kwa njia ya dijitali, uboreshaji wa vituo vya afya na mfumo wa Bima ya Afya ya Jamii, kama sehemu ya mabadiliko hayo.

Aidha, mkurugenzi huyo alisema Kenya imepanua uchunguzi wa magonjwa, uwezo wa utambuzi na ukabilianaji wa dharura, ikijifunza mengi kutoka kwa janga la COVID-19 na maambukizi mengine yaliyochupika.

Aliysema hayo huku Wizara ya Afya ikijiandaa kwa kongamano la Afya litakaloandaliwa kati ya Agosti 18-19, katika Jumba la Mikutano ya Kimataifa (KICC).

Share This Article