Kampuni ya Multi-Choice imezindua programu mpya ya GOtv streaming app, itakayowezesha wateja kutazama vipindi wanavyovienzi kutoka mahali popote kwa kutumia rununu.
Meneja Mkurugenzi Mkuu wa Multi-Choice Kenya Nzola Miranda, amesema wateja watapata burudani ya vipindi wavipendavyo, michezo, sinema na vipindi vingine kupitia kwa rununu.
GOtv Stream App inapatikana kwa wateja wanaotumia GOtv bouquets za GOtv Supa Plus, Supa, Max, Plus, na Lite.
“Huu ni ufanisi mkubwa katika jitihada zetu za kutoa burudani kwa mifumo ya kiteknolojia ili kuwapa wateja burudani isiyo kifani,” alisema Miranda.
“Tuko katika msimu wa sherehe za Krismasi na njia bora ya kusherehekea ni kutoa burudani kupitia kwa njai ya kipekee. Tunaongoza kuelezea hadithi mbalimbali humu nchini kwa kutumia teknolojia ya kisasa.”
Gotv Stream App inaruhusu mteja kupakua video 25 kwa wakati mmoja na kuzitazama kwa muda wa siku 30 huku video hizo zikitoweka saa 48 baada ya kutazama.
Pia wazazi wanaweza kuwazuia watoto kutazama sinema au vipindi vya watu wazima.