Waakilishi wa Kenya katika Ligi ya Mabingwa na kombe la Shirikisho Gor Mahia na Police FC, huenda wakahamishia mechi za mwezi ujao ikiwa mchujo wa mwisho.
Hii ni baada ya serikali kufunga uwanja pekee uliopo kwa sasa wa Nyayo ili kupisha ukarabati kwa maandalizi ya mashindano ya CHAN mwaka ujao.
Gor wameratibiwa kuwaalika mabingwa watetezi Al ahly tarehe 14 mwezi ujao katika ligi ya mabingwa, huku Police pia wakipangiwa kuanzia nyumbani dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe la Shirikisho Zamalek SC.
Huenda timu hizo za kenya zikaalazimika kucheza mechi zote nchini Misri ili kupunguza gharama.