Gavana wa zamani wa Samburu ahukumiwa miaka 8 gerezani

Tom Mathinji
1 Min Read
Gavana wa zamani wa Samburu Moses Lenolkulal

Gavana wa zamani wa Samburu Moses Kasaine Lenolkulal, ameingia katika kumbukumbu za historia ya taifa hili kwa kuwa Gavana wa kwanza aliyeondoka au aliye mamlakani kuhukumiwa kwa madai ya ufisadi chini ya katiba ya mwaka 2010.

Akitoa hukumu hiyo, hakimu mkuu Thomas Nzyoki, alimfunga Lenolkulal miaka nane gerezani, au alipe faini ya shilingi milioni 85.

Aidha hakimu huyo aliagiza kuwa Lenolkulal na Hesbon Ndathi, wanapaswa kulipa shilingi zingine milioni 83.

Tume ya kukabiliana na ufisadi hapa nchini EACC, imepongeza hatua hiyo, ikisema imewapa motisha ya kumfuata afisa mmoja mkuu kuhusiana na utajiri wake unaotiliwa shaka wa shilingi milioni 600.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na Joseph Riungu na Alex Akula, uliitaka mahakama kumfunga Gavana huyo wa zamani na washirika wake kifungo cha juu zaidi.

Hata hivyo upande wa utetezi ulitoa wito kwa Mahakama kuto-mfunga mteja wake, kwa kuwa hatua ya kusema anakabiliwa na shtaka, lilimtesa kimawazo gavana huyo wa zamani.

Washirika wake wanane wametozwa faini ya shilingi kati ya 700,000 na Milioni moja au kifungo cha miaka minne gerezani.

Lenolkulal amesema atakata rufaa katika Mahakamani ya kuu.

Mahama pia ilimzuia Lenolkulal na wenzake kushikilia wadhifa wowowte wa umma kwa kipindi cha miaka 10.

Website |  + posts
Share This Article