Gavana wa kaunti ya Nark Patrick Ole Ntutu, ametoa wito kwa madereva kuwa makini, ili kuzuia ajali za barabarani.
Wito wa Gavana huyo, unajiri siku moja baada ya watalii watatu wa kigeni na raia mmoja wa Kenya kufariki kwenye ajali ya barabarani, katika eneo la Katakala, katika barabara kuu ya Narok-Bomet.
Ajali hiyo ilitokea wakati gari la kuwabeba watalii aina ya Toyota, lilipogongana ana kwa ana na lori, na kuwaua wanne hao hapo hapo.
Huku akiomboleza na familia za waliopoteza wapendwa wao, Ntutu alitoa wito kwa madereva kuzingatia kikamilifu sheria za barabarani ili kuzuia ajali kama hiyo ya Jumatatu.
Kulingana na ripoti ya polisi, dereva wa gari hilo la kuwabeba watalii alikuwa kipita gari linginge bila kuwa makini, kabla ya ajali hiyo kutokea.