Gavana wa Kericho Eric Mutai atimuliwa

Dismas Otuke
1 Min Read

Bunge la kaunti ya Kericho siku ya Jumatano limekaidi agizo la mahakama na kumtimua Gavana Eric Mutai, kwa tuhuma za matumizi mabaya ya afisi na kukiuka katiba.

Waakilishi waodi 31 kati ya 47 wamepiga kura ya kumng’atua afisini Gavana huyo katika hoja iliyowasilishwa na MCA wa Sigowet Kiprotich Rogony.

Gavana huyo alidhani amepata afueni baada ya mahakama ya Kericho kutoa agizo la kusimamisha kutimuliwa kwake mapema Jumatano.

Hoja ya kumbandua Gavana huyo iliwasiliohswa katika bunge la Kericho tarehe 12 mwezi uliopita, huku Spika Patrick Mutai akitenga Oktoba 2 kuwa siku ya kuamuliwa kesi hiyo.

Gavana aliitwa kufika mbele ya bunge hilo leo lakini badala yake akakimbia mahakamani .

Gavana Mutai anatimuliwa kwa misingi ya kukiuka kanuni na matumizi mabaya ya afisi na kufuja pesa za kaunti.

Website |  + posts
Share This Article