Gavana Sakaja awataka wakazi wa Nairobi kujiepusha na siasa duni

Dismas Otuke
0 Min Read

Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja ametaka wakazi wa kaunti yake kujitenga na siasa duni za mgawanyiko na badala yake washirikiane kujenga taifa.

Sakaja amesema haya leo Jumapili aliposhiriki ibada katika kanisa la A.I.C Ziwani.

Aliwahakikishia wanaoishi katika nyumba za kaunti eneo la Ziwani kuwa hawatafurushwa.

Wengine waliohudhuria ibada hiyo ni Gavana wa Makueni Mutula Kilonzo Junior na Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen.

Share This Article