Gavana Nyaribo anusurika kubanduliwa madarakani

Martin Mwanje
1 Min Read
Amos Nyaribo - Gavana wa Nyamira

Gavana wa Nyamira Amos Nyaribo kwa mara nyingine amenusurika kura ya kumtimua madarakani. 

Hii ni baada ya wawakilishi wadi kukosa kufikisha theluthi mbili inayohitajika ya kumtimua Gavana huyo madarakani.

Wakati wa kikao kilichoandaliwa leo Jumanne, ni wabunge 22 waliopiga kura kuunga mkono hoja ya kumtimua Nyaribo madarakani.

Wawakilishi wadi 23 walihitajika kuunga mkono hoja hiyo ili kumtimua Nyaribo.

Wawakilishi wadi 12 walipiga kura kupinga hoja hiyo.

Nyaribo anakabiliwa na shutuma za kutumia vibaya madaraka na kuwa na mienendo mibaya.

Gavana huyo amekuwa akilumbana na wawakilishi wadi wa kaunti hiyo tangu alipoingia madarakani.

Share This Article