Gavana wa kaunti ya Kakamega Fernandes Baraza amelalamikia ongezeko ya visa vya utovu wa usalama akiahidi kushirikiana na vyombo vya dola kukabiliana na uhuni huo.
Baraza aliwataka Polisi kufanya uchunguzi wa kian na kuwachukualia hatua wote wanaohusika katika visa hivyo vya ukosefu wa usalama.
Baraza amesema haya siku ya Jumapili alihodhuria ibada katika kanisa la Christ Is The Answer Ministries (CITAM) mjini Kakamega.
Alimshutumu kiongozi wa wanawake wa kaunti hiyo Elsie Muhanda, kwa kuwatumia vijana kuzusha fujo na kuwataka polisi kumchukulia hatua.
Aidha,aliwaonya vijana dhidi ya kutumiwa na wanasiasa kwa njia zisizostahili.