Gavana wa kaunti ya Kakamega Fernandes Barasa, ameitaka Wizara ya Elimu kuingia kati kumaliza mgomo wa Walimu wa shule za upili na vyuo ambao umedumu kwa juma moja sasa.
Akizungumza Jumamosi katika kaunti yake ,Barasa amesema vita vya kibabe kati ya muungano wa walimu hao KUPPET na tume ya kuwaajiri walimu TSC, vinahatarisha viwango vya elimu ikizingatiwa kuwa muhula huu wa tatu ndio wa mtihani wa kitaifa KCSE.
“Ingawa vuta ni kuvute kati ya TSC na KUPPET itaishia kwa ushindi wa walimu ,wanafunzi ndio watakaoathiriwa zaidi ,hususan wale wanaojiandaa kwa mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE na kufanya kuula huu kuwa mfupi zaidikatika kelenda ya mwaka huu ya elimu.Wizara ya elimu yapaswa kutafuta suluhisho la haraka kumaliza mgomo huu.”akasema Gavana Barasa
Wanlimu wa shule za msingi wa chama cha KNUT walifutilia mbali mgomo wa kitaifa uliokuwa uanze Jumapili iliyopita baada ya kuafikiana na tume ya TSC, huku wale wa KUPPET wakikosa kufungua shule baada ya TSC kushindwa kutekeleza matakwa yao.
Walimu walio katika muungano wa KUPPET wanadai kutekelezwa kikamilifu kwa mwafaka wa nyongeza ya mshahara wa mwaka 2021/2025 kikamilifu,kuafikia kwa makubaliano mapya ya nyongeza ya mshahara,bima bora ya afya,kupandishwa vyeo kwa walimu waliokwama kwa muda mrefu na kuwasilishwa kwa makato yote ambayo hayajawalishwa licha ya kuondolewa katika mishahara ya walimu miongoni mwa matakwa mengine.
Mgomo huo unatarajiwa kuingia wiki ya pili Jumatatu ijayo endapo suluhu haitapatikana kufikia kesho.