Gavana Achani akariri kuboresha huduma ya afya Kwale

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali ya Kaunti ya Kwale imetangaza kusitisha ujenzi wa vituo vipya vya Afya na badala yake itaendelea kuboresha vituo vya Afya vilivyoko Kwa sasa, ili kuinua viwango vya huduma za Afya katika Kaunti ya kwale.

Kufikia sasa, Serikali ya Kaunti ya Kwale imeongeza idadi ya vituo vya Afya kutoka 35 hadi vituo 165 pamoja na ,kuajiri wahudumu wa afya 1,800 pamoja na ujenzi wa vyumba vya wagonjwa mahututi almaarufu ICU katika hospitali ya rufaa ya Msambweni.

Akizungumza alipokuwa akizindua usambazaji wa hundi za basari Kwa wanafunzi wa shule za upili huko Kinondo eneo bunge la Msambweni, Gavana wa Kaunti ya Kwale Fatuma Achani alisema kuwa analenga kuhakikisha kuwa vituo vya afya katika kaunti ya kwale vina dawa za kutosha , vifaa hitajika pamoja na wahudumu wa afya wa kutosha,kutoa huduma bora za matibabu kwa wakazi wa Kwale.

Aidha kiongozi huyo amekosoa vikali wanaoeneza habari potofu kuhusu sekta hio ya Afya, akisema Serikali yake imejizatiti ili kuhakikisha inakabiliana na changamoto zinazoikumba sekta ya afya

Share This Article