Gavana wa kaunti ya Wajir Ahmed Abdullahi amewaasa vijana dhidi ya uharibifu wa mali wakati maandamano,akisema kuwa hali hiyo huenda ikasambaratisha taifa.
Gavana huyo alisema nchi ya Kenya haipaswi kufuata mkondo wa mataifa kama vile Somalia na Sudan, ambayo yameporomoshwa na vita vya kimbari.
Akiunga mkono haki za vijana wa Gen Z kuandamana kwa amani ,Abdulahi alisema mkondo wanaoufuata vijana hao ni hatari na huenda ukasababisha machafuko.
Badala yake Gavana huyo amewataka vijana hao kufanya majadiliano kuhusu maswala yanayowasibu .