Gachagua atoa wito kwa Wakenya kudumisha amani

Tom Mathinji
1 Min Read
Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua ameendeleza wito wake wa kuwataka Wakenya kudumisha amani, na kufanya kazi kwa bidii wakati huu mgumu wa kiuchumi.

Akizungumza alipohudhuria ibada ya Jumapili katika kanisa la Brotherhood Fellowship Kahawa West, kaunti ya Nairobi, Gachagua alisema bila kuzingatia yale ambayo yanaendelea, ni muhimu kudumisha amani hapa nchini.

Wakati huo huo, Gachagua aliwahimiza maafisa wa serikali kuendeleza miradi aliyoanzisha akiwa serikalini kwa manufaa ya wananchi.

Aliwahimiza maafisa hao kuonyesha utu kwa wakenya hasaa kuhusu kuwahamisha wananchi kwa lazima.

Aliunga mkono uamuzi wa mahakama, uliotaka wale wote wanaohamishwa kwa lazima kulipwa fidia.

Gachagua alikuwa ameandamana na viongozi kadhaa, wakiwemo Wanjiku Muhia,(Kipipiri) James Gakuya (Embakasi Kaskazini) Samuel Parashina,(Kajiado Kusini), Benjamin Gathiru Mejja Donk (Embakasi ya kati), Seneta wa Murang’a Joe Nyutu, na aliyekuwa mwakilishi mwanamke wa Laikipia Cate Waruguru miongoni mwa wengine.

Share This Article