Gachagua ataka mdahalo wa chaguzi za 2027 na 2032 ukome

Martin Mwanje
1 Min Read
Naibu Rais Rigathi Gachagua ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa kusitisha mdahalo wa kugawana nyadhifa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 na 2032.
Badala yake, anataka juhudi zote kuelekezwa kwa utekelezaji wa manifesto ya Rais William Ruto.
Naibu Rais ametoa wito kwa viongozi kusitisha mdahalo huo ili kiongozi wa nchi afanikiwe katika ajenda yake ya maendelo.
“Wakenya wanataka maendeleo wala si siasa au kuonyesha jinsi ulivyo tajiri,” alisema Gachagua wakati wa mahojiano ya pamoja na vyombo vya habari kutoka eneo la Mlima Kenya vinavyotangaza katika lugha ya mama jana Jumapili usiku.
“Vyongozi wa kisasa na maafisa wa umma wanapaswa kuangazia kuelekeza shabaha yao kwa kuwafanyia kazi Wakenya ili Rais aweze kufanikiwa katika mpango wake wa maendeleo. Hebu tuepukane na mdahalo wa chaguzi za 2027 na 2032. Badala yake, nguvu zote zinapaswa kuelekezwa kwa kutekeleza mamlaka ya nyadhifa za sasa na ofisi wanazoshikilia.”
Share This Article