FOCAC 2024: China yaahidi kuimarisha uhusiano wa kiuchumi, biashara na Afrika

Tom Mathinji
5 Min Read

China imeelezea nia yake ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na nchi za Afrika kwa manufaa ya pande zote mbili.

Maafisa kutoka baraza la China la kukuza biashara ya kimataifa (CCPIT) walisema kuwa uhusiano wa kiuchumi kati ya China na Afrika umenawiri kwa miaka nyingi, na kuifanya China kama mshirika mkubwa wa biashara na mkopeshaji wa Afrika.

Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo Zhang Shaogang, anasema mafanikio haya, kwa sehemu kubwa, imechangiwa na jukwaa la ushirikiano wa China na Afrika (FOCAC). Anaamini kuwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000, FOCAC imebadili biashara na uchumi. Jukwaa hilo limesababisha ufadhili mkubwa wa kifedha kutoka China, ikiwa ni pamoja na uwekezaji ambao umesaidia kukuza maendeleo ya kiuchumi katika nchi za Afrika.

Zhang aliisifia FOCAC kwa lengo lake la kuboresha muunganisho wa miundombinu, ambayo ni kichocheo muhimu wa ushirikiano wa biashara na kiuchumi. Alitaja miradi kama barabara, reli, na vituo vya nishati ambavyo vimetekelezwa na hivyo kuvimeimarisha vifaa vya biashara.

Aidha, aliipongeza jukwaa la FOCAC kwa kuwezesha mazungumzo kati ya China na Afrika. Alisema jukwaa hilo linatoa nafasi ya majadiliano ya sera, kuwezesha mpangilio bora wa mikakati ya maendeleo na kuongeza ufanisi wa mikataba ya biashara na uwekezaji.

Zhang alisisitiza kuwa serikali ya China inathamini sana ushirikiano kati ya jumuiya za wafanyabiashara wa China na Afrika. Alitoa hakikisho kwamba China itaendelea kutoa msaada kwa Afrika huku akitoa wito wa kukuza ujumuishaji wa kiviwanda na katika usambazaji.

“China itapanua ufunguzi wa taasisi kwa Afrika, na kukuza ushirikiano katika mnyororo wa viwanda na ugavi, kukuza ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo ya fedha kati ya China na Afrika, pamoja na kutoa faida za pamoja kwa wote. Hii itachangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Afrika.” Alisema

Zhang pia aliwataka wajasiriamali kutoka China na Afrika kutumia majukwaa ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, kama vile China International Supply Chain, ili kuboresha ujumuishaji wa minyororo ya viwanda na usambazaji. Alisisitiza umuhimu wa kupinga kwa pamoja uzuizi na kudumisha minyororo thabiti ya viwanda na usambazaji.

Akibainisha kuwa China kwa sasa inaimarisha nguvu za uzalishaji wa hali ya juu huku Afrika ikitathmini kikamilifu njia yake ya kujiendeleza, Zhang alitoa wito kwa pande hizo mbili kuungana ili kuafikia mafanikio makubwa.

“Kuna uwezekano mkubwa wa ushirikiano kati ya Afrika na China katika maeneo kama vile maendeleo ya kijani na akili bandia. Ni matumaini yetu kuwa wajasiriamali kutoka China na Afrika wanaweza kushirikiana katika viwanda vinavyochipukia na kufanya kazi kwa pamoja ili kukuza maendeleo ya viwanda,” alisema

Alizungumza wakati ambapo mkutano wa wajasiriamali ulipangwa kufanyika mwezi huu, ambapo wajasiriamali kutoka China na Afrika watajadili fursa za ushirikiano kutokana na hatua mpya zilizotangazwa katika mkutano huo.

Sun Xiao, msemaji wa baraza hilo la CCPIT, alielezea hisia kama hizo, akisema kuwa kupitia FOCAC, biashara za Kichina zimehimizwa kuwekeza Afrika, na kusababisha uundaji wa nafasi za ajira na uhamishaji wa teknolojia na ujuzi. Ushirikiano huu unalenga kuambatana na malengo ya maendeleo ya Afrika na kukuza ukuaji endelevu na wa manufaa ya kiuchumi.

Kama taasisi, Sun alisema CCPIT inataka kutoa msaada muhimu kwa makampuni ya Afrika ili kuyasaidia kustawi.

“CCPIT itaimarisha ushirikiano na taasisi sawia barani Afrika ili kuimarisha na kuboresha mnyororo wa viwanda na ugavi, kwa lengo la kutoa michango zaidi kwa uchumi wa dunia kuwa wazi,” alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

“Katika kukuza maendeleo ya viwanda vinavyojitokeza, China na Afrika zimepata matokeo makubwa katika maeneo kama vile uchumi wa dijitali na maendeleo ya kijani,” aliongeza.

Alisema China imeisaidia Afrika kikamilifu katika ujenzi wa miundombinu yake ya kidijitali.

“Tangu kuanzishwa kwa FOCAC, makampuni ya China yamesaidia katika kujenga na kuboresha miundombinu muhimu ya mawasiliano yenye urefu wa kilomita 150,000, na kutoa huduma za mtandao kwa watumiaji milioni 700,” alielezea.

Sun aliendelea kusema kuwa China ni mshirika muhimu wa ushirikiano kwa Afrika katika suala la mabadiliko ya nishati, na kwa sasa itekeleza miradi nyingi ya nishati safi ndani ya mfumo wa FOCAC.

“Tunaunga mkono nchi za Afrika katika kutumia uwezo walio nao katika nishati ya jua, maji, na nishati ya mvuke ili kuafikia maendeleo ya kijani, viwango vya kaboni vya chini, na ya hali ya juu,” alisema, akisisitiza kuwa mipango hii, pamoja na mengine yanaojitokeza, yatachangia mafanikio ya kiuchumi ya Afrika.

Share This Article