FKF yaunda jopo la watu saba kuendesha shughuli za soka humu nchini

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirikisho la soka nchini FKF limebuni kamati ya mpito ya watu saba kusimamia uendeshaji wa shughuli za kandanda.

Kamati hiyo ilibuniwa wakati wa kikao cha baraza kuu NEC tarehe 21 mwezi uliopita na itaongozwa na Naibu Rais wa FKF McDonald Mariga, akisaidiwa na mwakilishi wanawake
Kerubo Momanyi.

Wanachama wengine ni mwakilishi wa baraza kuu eneo la Upper Rift Bernard Lagat, ambaye atakuwa Katibu huku wanachama wengine wakiwa mwakilishi wa NEC eneo la mashariki Charles Njoka Njagi,
wenzake Robert Macharia wa Central ,Ahmedqadar Mohammed Dabar wa kaskazini mashariki na Peter  Kamau wa Lower Rift.

Majukumu ya kamati hiyo ni pamoja na kuanzisha ukaguzi wa fedha,ukaguzi wa wafanyikazi na idara zilizopo katika shirikisho hilo,kutathmini sera zilizopo na maungufu yake na kuhakisha shughuli za shirikisho zinaendelea bila hitilafu.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *