Kikao maalum cha FKF kimeteua Bodi ya wanachama saba itakayosimamia uchaguzi wa Shirikisho hilo unaotarajiwa kuandaliwa
Bodi hiyo iliyotangazwa Jumamosi inawajumuisha wanachamawatano na wengine wawili wakiwa wanachama wa akiba.
Hesbon Owila ataongoza bodi hiyo huku wanachama wengine wakiwa James waindi,Alfred Ng’ang’a,Dan Mule na Merceline Sande .
Farida Juma na Robert Asembo watakuwa wanachama wa ziada katika bodi hiyo.
Mkutano huo maalum wa SGM umefanyika baada ya kuahirishwa mara kadhaa na mahakama.
Uchaguzi wa FKF unatarajiwa kuandaliwa mwezi Oktoba mwaka huu.