Shirikisho la kandanda ulimwenguni (FIFA) limetangaza kuwa litatoa pete kwa kila mchezaji wa timu itakayotwaa Kombe la Dunia katika fainali ya Jumapili hii mjini New York Marekani.
Timu itkayoshinda fainali kati ya Argentina na Uhispania itapokea pete 30,moja kwa kwa kila mchezaji na afisa wa benchi ya kiufundi kuongezea kwa medali za dhahabu watakazovishwa na kombe la kifahari.
Aidha, FIFA imetangaza kuwa pete nyingine 1,996 zitauziwa mashabiki kama kumbukumbu ya Kombe la Dunia.
Mabingwa wa Kombe hilo watatuzwa shilingi bilioni 6.47,nafasi ya pili shilingi bilioni 4.27, huku mshindi baina ya Ufaransa na Uingereza, Jumamosi akitia kibindoni shilingi 3.75 ,na timu ya nne iondoke na shilingi bilioni 3.49.
Timu zilizobanduliwa katika kwota fainali zikiwa;Morocco, Ubelgiji, Norway na Uswizi, zitapokea shilingi bilioni 2.46 kila moja .
Mataifa yaliyobanduliwa katika raundi ya 16 yatatuzwa shilingi bilioni 1.94 kila moja .
Timu zilizomaliza nafasi za 17 hadi 32 zitapokea shilingi bilioni 1.42, huku mataifa yaliyoaga mashindano katika hatua ya makundi yakizawadiwa shilingi bilioni 1.16 kila moja.