Misri kutuma ombi la kuandaa AFCON mwaka 2028

Misri iliandaa AFCON kwa mara ya mwisho mwaka 2018.

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama cha soka nchini Misri (EFA) kimetangaza azma ya kutaka kuandaa fainali za Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2028 .

Kulingana na mwanachama wa halmashauri ya EFA, Hamada El-Sherbiny, Misri inatafakari kuwa mwenyeji wa kipute cha AFCON .

Yamkini EFA imechochoewa na matokeo mazuri ya timu ya taifa katika fainali za kombe la Dunia zinazoendelea ambapo walicheza hadi hatua ya 16 bora.

Misri iliandaa AFCON kwa mara ya mwisho mwaka 2018.

TAGGED:
Share This Article