Fid Q akamilisha kozi fupi ya usimamizi wa sanaa

Marion Bosire
1 Min Read
Fid Q akipokezwa cheti na Mwana FA

Farid Kubanda maarufu kama Fid Q ni msanii wa muziki mtindo wa HipHop nchini Tanzania na ni mmoja wa waliofuzu baada ya kukamilisha kozi fupi kuhusu uongozi, biashara na utawala katika Sanaa.

Kozi hiyo ilitolewa na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo almaarufu TaSUBa.

Sherehe ya kufuzu iliandaliwa Disemba 8, 2023 na ilihusu wanafunzi 16 wakiwemo 7 wa kike na 9 wa kiume.

Waliofuzu walikabidhiwa vyeti vya kuhitimu na baadhi yao ni Viongozi wa mashirikisho na vyama vya Sanaa nchini.

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo,Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA ambaye pia ni mwanamuziki alikuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo ya 34 ya ya aina yake.

Kufikia sasa taasisi ya sanaa na utamaduni Bagamoyo imetoa vyeti vya astashahada na stashahada kwa watu 270.

Mwana FA alisema kwamba huenda kanuni zikabadilishwa hivi karibuni ili kuhakikisha kwamba yeyote anayewania wadhifa kwenye mashirikisho ya wasanii awe na cheti cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo.

Kulingana naye kushiriki shughuli za sanaa kwa muda mrefu hakumpi mtu uwezo wa uongozi ila anafahamu tu kuhusu kinachofanyika katika sanaa lakini anakosa uwezo wa uongozi.

Share This Article