Familia zaidi ya 700 zimelazimishwa kuhama makwao baada ya nyumba zao kusombwa na maji kufuatia kufurika kwa mto Ewaso Nyiro uliovunja kingo zake.
Kulingana na na shirika la msalaba mwekundu familia 708 zilikuwa zimesombwa na maji eneo la Merti kaskazini na kusini kaunti ya Isiolo.
Kulingana na wizara ya usalama wa ndani watu 291 wameripotia kufariki kutokana na mafuriko kufikia Alhamisi Mei 16, huku wengine 75 wakiwa hawajulikani waliko na wengine 188 wakiuguza majereha.
Jumla ya familia 55,631 zimehamishwa makwao tangu kuanza kwa mafuriko yalisababishwa na mvua kubwa kote nchini Kenya.