Fahamu ndege aina ya Dornier 228-202k

Tom Mathinji
3 Min Read
Helikopta aina ya Dornier 228- 202k.

Tarehe 10, Juni 6,2024, makamu wa rais wa Malawi Saulos Chilima na wengine tisa walifariki katika ajali ya ndege ya kijeshi iliyoanguka katika msitu wa chikangawa kaskazini mwa taifa hilo baada ya kupoteza mawasiliano na kituo cha ndege cha Mzuzu.

Kufuatia ajali hiyo, maswali mengi yameibuka kuhusu ubora wa aina hizo za ndege.

Hii leo kwenye makala ya Mwanga wa wiki, tunaangazia ndege aina ya Dornier 228-202k iliyomuua Chilima.

Kwa mujibu wa mtandao unaoangazia safari za ndege (Avation analytic Cirium), Malawi ilinunua ndege tatu za Dornier kati ya mwaka wa 1986 na 1989 kutoka kampuni ya Dornier ya Ujerumani.

Kampuni hiyo ilizinduliwa mwaka wa 1914 na Claudius Dornier na kufungwa mwaka wa 2002 kwa sababu ya changamoto za kifedha.

Katika kipindi hiki, zaidi ya ndege 1,000 ziliuzwa kote duniani.

Dornier 228-202k ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 18 na marubani wawili.

Uzito wake wa kupaa ulikuwa kilo 6,200 na mwendo kasi wa kilomita 430 kwa saa ikiwa futi 25,000 angani huku bei yake ikikisiwa kuwa takribani dola za kimarekani million 2.3 ya enzi hizo.

Kulingana na rekodi kote duniani, Ndege zenye miundo tofauti ya Dornier zimesababisha ajali 96 na kuua takriban watu 218 nayo yenye muundo wa 228-202k zikiua watu 12 kati ya mwaka wa 2008 na 2024 nchini Malawi(10) na Chile (2).

Ajali zingine ambapo hazikuua watu ni zile zilizotokea Afrika ya kati, Uphilipino, Nepal, Bara Hindi na Austrelia.

Miundo mingine ya Dornier iliyosababisha ajali ni kama ifuatavyo; Tarehe 24 Nov 2019 Dornier 228-201 ilianguka mjini Goma DRC na kuua watu 27.

Nchini Nigeria Dornier 228-212 za jeshi zilianguka na kuua watu 13 na 7 majimboni Benue na Kaduna mnamo Sept, 2006 na Agosti 2015 mtawalia.

Ajali zingine za ndege hiyo hapa Afrika ni ile ya Agosti, 1999 iliyoua abiria 18 nchini Cape Verde na ya mwezi Septemba mwaka wa 2020 mjini Pibor Sudan Kusini iliyoua mtu mmoja.

Tangu mwaka wa 1992 hadi 2024, ajali za Dornier zisizo na vifo zilitokea Nigeria mara tatu, DRC mara mbili, Somali moja na Sao Tome na Principe moja.

Nje ya Afrika, Dornier iliua watu 11 magharibi mwa bara Hindi mwaka wa 1989. Nchini Nepal, watu 19, 14 na 15 walikufa mwaka wa 1993, 2010 na 2012 mtawalia.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *