EU yatoa wito wa ‘haki’ baada ya vurugu nchini Syria

Martin Mwanje
1 Min Read

Umoja wa Ulaya (EU) umepongeza hatua ya Syria kubuni kamati ya kubaini ukweli ili kuchunguza wimbi la hivi karibuni la vurugu zilizosababisha maafa, na kutoa wito kwa waliotekeleza vurugu hizo “kuwajibishwa.”  

“Tunalaani vikali mashambulizi yaliyotekelezwa na wanamgambo wanaomuunga mkono Assad dhidi ya vikosi vya usalama,” ilisema EU kwenye taarifa iliyotolewa jana Jumanne jioni.

“Pia tunalaani vikali uhalifu wa kutisha uliotekelezwa dhidi ya raia, yakiwemo mauaji ya moja kwa moja, mengi ambayo yamedaiwa kutekelezwa na makundi yenye silaha yanayounga mkono vikosi vya usalama vya mamlaka za mpito .”

Wimbi la vurugu lilianza Alhamisi iliyopita hasa katika eneo la Mediterania la kabila la wachache la Alawite, likiwa baya zaidi tangu kubanduliwa kwa Rais wa zamani wa Syria Bashar al-Assad mwezi Disemba mwaka jana.

Vikosi vya usalama na makundi washirika yameua raia wasiopungua 1,225 tangu Alhamisi iliyopita, kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu linalojiita Syrian Observatory for Human Rights.

 

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article