Kituo maalum kinachosimamia usalama na hali ya dharura iliyotangazwa katika jimbo la Amhara kaskazini magharibi mwa Ethiopia, limeondoa amri ya kutotoka nje iliyowekwa katika jimbo la Amhara.
Amri hiyo iliangazia usalama katika barabara kuu inayounganisha miji ya Debre Berhan na Dessie ikisema imeimarika.
Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya gazeti linalomilikiwa kibinafsi la Addis Standard.
Kituo hicho cha kusimamia usalama kimesema kwamba amri hiyo imeondolewa kuanzia Jumamosi Aprili 6.
”Uamuazi wa kuondoa amri hiyo ulitokana na hali ya usalama kuimarika na vile vile ombi rasmi kutoka kwa jamii ya eneo hilo, ‘ gazeti hilo liliripoti.
Mnamo Februari 24 KItuo hicho Kilitoa amri ya kupiga marufuku safari zote kwenye barabara hiyo inayounganisha miji hiyo miwili baada ya wapiganaji wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Fano kuuawa raia wanane.
Kundi hilo la Fano limeshutumiwa kwa kutekeleza maovu dhidi ya raia na kupora mali.