Ethiopia imeomba mkopo wa dola milioni 700 za Marekani kutoka kwa Benki ya Dunia, kufadhili miradi muhimu ya muundo msingi ikiwemo kufufua benki ya kitaifa inayomilikiwa na serikali inayoyumba .
Benki ya kitaifa ya Ethiopia inakabiliwa na misukosuko kutokana na madeni mabaya ya wateja waliokosa kulipa mikopo.
Pesa hizo pia zitawezwa katika ufufuzi wa sekta kadhaa za serikali zinazochechemea.