Kampuni ya mawasiliano ya kutumia satelaiti kukusanya habari na mawasiliano iliyoko eneo la Ngomeni, kaunti ya Kilifi imekabidhi idara ya polisi nchini kituo kipya cha polisi cha Ngomeni.
Hatua hiyo inalenga kuimarisha zaidi usalama eneo hilo.
Kamishena wa kaunti ya Kilifi Josephat Biwott akiandamana na wakuu wengine kutoka idara ya polisi, ameipongeza kampuni hiyo kwa jitihada hizo huku akidokeza kuwa kituo hicho kitaanza kazi mara moja.
Kituo hicho cha kisasa kinatazamiwa kuboresha usalama katika eneo hilo la Ngomeni.