Bilionea wa kampuni ya Tesla Elon Musk, ametangaza kujiondoa kwenye serikali ya Rais Donald Trump, wa Marekani baada ya kukamilisha wajibu kama mjumbe maalum.
Musk ambaye amekuwa mshauri mkuu wa Trump alitangaza kuondoka kwake serikalini bila ya kufanya mazungumzo na Rais Trump.
Serikali ya Marekani imepiga hatua kubwa katika kipindi ambacho Musk amekuwa mshauri wa serikali kwa masuala kadhaa ya kiuchumi.
Hata hivyo Musk alifarakana na Mawaziri kadhaa wa serikali ya Trump kutokana na msimamo na baadhi ya sera zake.
Muda wa kuhudmu kwa Musk unakamilika Mei 30 .