Elfyn Evans atwaa ubingwa wa WRC Safari Rally

Dismas Otuke
1 Min Read

Elfyn Evans wa kampuni ya magari ya Toyota GR Yaris,akishirikiana na mwelekezi wake Scott Martin, ndiye bingwa wa mashindano ya WRC Safari Rally mwaka huu.

Evans alitwaa ushindi wa Safari Rally kwa mara ya kwanza akimuacha Ott Tänak, wa kampuni ya magari ya Hyundai kwa dakika 1 sekunde 9.9.

Raia huyo huyo wa Uskochi, alichukua uongozi wa mashindano hayo siku ya Ijumaa na kuduisha uongozi huo.

Thierry Neuville wa Hyundai alimaliza wa tatu.

Gus Greensmith akishirikiana na Jonas Andersson walishinda akitengo cha WRC2.

Kampuni ya Toyota ilinyakua ubingwa wa jumla ikufuatwa na Hyundai, huku Ford ikichukua nafasi ya tatu.

Carl Flush Tundo na Jeremmy Wahome ndio Wakenya walionyakua nafasi bora wakifuatana katika nafasi za 14 na 15 mtawalia.

Mkondo wa Kenya ambao umekuwa wa tatu, utakaofuatwa na ule wa WRC Rally Islas Canarius, utakaondaliwa Uhispania kati ya tarehe 24 na 27 mwezi ujao.

Website |  + posts
Share This Article