Mwenyekiti wa KEPSHA Johnson Nzioka afariki kwenye ajali

Nzioka alifariki jana Jumapili, Feruari 16, 2025 kufuatia ajali mbaya iliyotokea kwenye barabara ya Mombasa Road inayojulikana kuwa na shughuli nyingi.

Martin Mwanje
1 Min Read
Johnson Nzioka - Mwenyekiti wa KEPSHA aliyefariki kwenye ajali Mombasa Road

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wakuu wa Shule za Msingi nchini Kenya (KEPSHA) Johnson Nzioka ameaga dunia. 

Nzioka alikumbana na mauti kutokana na ajali ya barabarani iliyotokea kwenye barabara ya Mombasa Road jana Jumapili.

Waziri wa Elimu Julius Migos na Chama cha Walimu nchini (KNUT) ni miongoni mwa waliomwomboleza marehemu ambaye alihudumu kama Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Donholm.

“Alikuwa mwalimu na kiongozi mwenye umaizi na aliyefanya kazi kwa kujitolea, aliyeutakia mfumo wetu wa elimu mema,” alisema Migos katika risala zake za rambirambi.

“Kama mwenyekiti wa KEPSHA, Nzioka alikuwa makini katika kuimarisha wajibu wa usimamizi wa shule ili kupata matokeo bora ya elimu.”

Katibu Mkuu wa KNUT Collins Oyuu amemwelezea marehemu kama kiongozi shupavu aliyekuwa ana ujuzi wa kipekee wa kidiplomasia.

“Atakumbukwa kwa uzungumzaji wake wa unyenyekevu lakini wa wazi, hasa wakati wa kutafuta amani miongoni mwa wanachama wake,” alisema Oyuu.

Website |  + posts
Share This Article