Nahodha wa Nigeria William Troost-Ekong alitawazwa mchezaji bora wa makala ya 34 ya kipute cha AFCON nchini Ivory Coast.
Mshambulizi wa Equitorial Guinea Emilio Nsue Lopez, alinyakua tuzo ya mfungaji bora kwa mabao matano, huku Ronwen Williams wa Afrika Kusini akitawazwa kipa bora .
Ivory Coast ilinyakua tuzo ya timu yenye nidhamu bora.
Simon Andingra wa Ivory Coast alitunukiwa tuzo ya chipukizi bora wa mashindano hayo akiwa na umri wa miaka 22.
Kwa jumla magoli 119 yalifungwa kutokana na mechi 52.