EACC yawakamata wafanyakazi wa KPLC kwa tuhuma za ufisadi

Wafanyakazi waliokamatwa ni Jeremiah Onchuru Omwenga, Jeremiah Omondi Masiwa, na John Mutuku Mutua. 

Martin Mwanje
1 Min Read
Washukiwa wa ufisadi waliokamatwa na EACC
Mamlaka ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imewakamata wafanyakazi watatu wa kampuni ya umeme nchini, KPLC kwa madai ya ufisadi. 
Wafanyakazi waliokamatwa ni Jeremiah Onchuru Omwenga, Jeremiah Omondi Masiwa, na John Mutuku Mutua. 
Omwenga, mhasibu kwenye jumba la Electricity, anatuhumiwa kwa kuitisha hongo ya shilingi 200,000 ili kubadili bili ya umeme iliyozozaniwa ya shilingi 346,000.
“Kufuatia malalamishi, Tume ilifanya operesheni iliyosababisha kukamatwa kwake wakati akipokea fedha hizo,” ilisema EACC kwenye taarifa.
Katika mtaa wa Woodley, Nairobi, tume hiyo iliwakamata Masiwa na Mutua wakati wakipokea hongo ya shilingi 10,000 kutoka kwa mkazi aliyejiunganishia umeme kinyume cha sheria.
Washukiwa hao watatu walipelekwa katika kituo cha polisi cha Integrity kabla ya kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi 50,000 kila mmoja wakisubiri kuhitimishwa kwa uchunguzi kuhusiana na madai hayo.
Website |  + posts
Share This Article