Mwenyekiti wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) Dkt. David Oginde, amewahimiza wahasibu na wataalam wengine kuzingatia maadili na kukabiliana na ufisadi, akionya kuwa utaalam unatumika kufanikisha uhalifu wa kiuchumi.
Akizungumza kwenye mkutano wa wajumbe wa Taasisi ya Wahasimu walioidhinishwa wa Umma (ICPAK) Jijini Mombasa, Dkt Oginde alisisitiza kuwa maadili huanza na maamuzi ya mtu binafsi na yanapaswa kudhihirishwa kupitia shughuli za kila siku za kitaalam.
“Maadili hayalazimishiwi mtu, ni uamuzi wa mtu binafsi,” alisema mwenyekiti huyo.
Aidha, alielezea wasiwasi kuhusu kujumuishwa kwa wataalam, wakiwemo wahasibu katika visa vya ufisadi, akidokeza kuwa ujuzi walio nao una uwezo wa kusababisha kutogunduliwa haraka kwa ufisadi.
Alitoa changamoto kwa wahasibu kutambua jukumu lao muhimu la kulinda uwajibikaji wa kifedha na kuzuia ufisadi.
Kulingana na Dkt. Oginde, wadhifa wa wahasibu hao unaweza linda maadili ya taasisi au kufanikisha utekelezaji makosa.