Watu 10 wafariki kwenye maandamano nchini Guinea

Waandamanaji hao wanapinga marufuku dhidi ya uchimbaji dhahabu katika eneo la Sigur.

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu 10 wafariki kwenye maandamano nchini Guinea.

Watu 10 wamefariki na 13 kujeruhiwa kwenye makabiliano kati ya waandamanaji na maafisa wa usalama nchini Guinea, kulingana na serikali ya taifa hilo.

Waandamanaji hao wanapinga marufuku dhidi ya uchimbaji dhahabu katika eneo la Sigur, na walikabiliana na polisi waliokuwa wakitekeleza marufuku hayo.

Kulingana na taarifa ya polisi, waandamanaji hao waliweka vizuizi barabarani kuzuia doria za maafisa wa polisi, huku hali hiyo ikigeuka kuwa makabiliano ya risasi. Hata hivyo taarifa hiyo haikuelezea ni nani alifyetua risasi.

Miongoni mwa waliofariki ni raia watano wa kigeni ambao bado hawajatambuliwa, huku waliojeruhiwa wakijumuisha waandamanaji na maafisa wa usalama.

Guinea ilipiga marufuku uchimbaji madini Novemba 2 kwa madai kwamba wachimbaji dhahabu walikosa kutekeleza sheria zilizowekwa na hivyo kusababisha uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na ardhi ya kilimo, mito na utandu wa mimea.

TAGGED:
Share This Article