DRC yapokea awamu ya kwanza ya chanjo ya Mpox

Tom Mathinji
1 Min Read

Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, imepokea awamu ya kwanza ya chanjo za kukabiliana na ugonjwa wa Mpox.

DRC ambayo ndio chimbuko la ugonjwa wa Mpox, imenakili visa 19,000 vya maambukizi ya ugonjwa huo, huku vifo 650 vikithibitishwa nchini humo.

“Chanzo hizo zimewasili DRC. Zimepelekwa kuhifadhiwa na kamapeni ya utoaji chanjo inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu,” alisema mkuu wa halmashauri ya kukabiliana na dharura za afya wa Muungano wa Ulaya Laurent Muschel.

Waziri wa afya wa DRC Samuel-Roger Kamba na Laurent Muschel, walipokea dozi 99,100 za chanjo hizo katika uwanja wa ndege wa Kinshasa, alisema mwanahabari wa shirika la AFP.

“Chanjo hizi ni za bei ghali sana, hatuwezi nunua kama taifa,” alisema waziri Kamba.

Ugonjwa wa Mpox husambazwa kwa binadamu kutoka kwa wanyama walio na ugonjwa huo, na pia unaweza sambazwa kutoka kwa binadamu hadi kwa binadamu.

Hadi kufikia sasa, mataifa 13 barani Afrika yamenakili ugonjwa huo. Nchi hizo ni pamoja na Burundi, Congo-Brazzaville na Jamuhuri ya Afrika ya kati, kulingana na kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika CDC.

Shirika la Afya duniani WHO, lilitangaza ugonjwa huo kuwa dharura ya afya ya umma mnamo Agosti 14, 2024.

TAGGED:
Share This Article