Dkt Ronoh: Serikali itaendelea kupiga jeki sekta ya Majani chai

Tom Mathinji
1 Min Read
Katibu katika wizara ya kilimo Dkt. kiprono Rono.

Wizara ya kilimo imejitolea kuhakikisha sekta ndogo ya Majani Chai inastawi, ili iweze kuchangia katika maendeleo ya uchumi wa kijamii wa taifa hili.

Akizungumza aliposhiriki meza ya mazungumzo na wakurugenzi wa kampuni za Majani Chai eneo la West Rift, katibu katika wizara ya kilimo Dkt. Kipronoh Ronoh, alisema ipo haja ya kuwezesha sekta hiyo ndogo kupata faida, ili iendelee kutoa nafasi za ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.

Katika mkutano huo, Dkt Ronoh aliwafahamisha wakurugenzi hao kuwa, wizara yake itashirikiana nao, kuwanufaisha wakulima wa Majani Chai na taifa hili kwa jumla.

Wizara ya kilimo imeahidi kuimarisha sekta ndogo ya Majani Chai.

“Wizara ya kilimo tayari imeanzisha mipango ya kuinua sekta ndogo ya Majani Chai, inayojumuisha utoaji wa mbolea ya gharama nafuu na vifaa vya kuongeza dhamani kwa Majani Chai,” alisema Dkt. Ronoh.

Wakati huo huo, Katibu huyo lisema maswala yote yaliyoibuliwa na wakurugenzi hao yatashughulikiwa kwa haraka, kupiga jeki ukuaji wa sekta hiyo.

Wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Afisa Mkuu Mtendaji wa bodi ya Majani Chai ya Kenya Willy Mutai, miongoni mwa wengine.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *