Dkt. Omollo: Tuwape motisha wanafunzi wetu kuendelea na masomo

Tom Mathinji
2 Min Read
Katibu katika wizara ya Usalama wa Taifa Dkt. Raymond Omollo.

Katibu katika wizara ya Usalama wa Taifa Dkt. Raymond Omollo, ametoa wito kwa wazazi, walimu na viongozi wa jamii kushirikiana kukabiliana na changamoto ya wanafunzi kuacha masomo, akisema hatua hiyo itadumaza mustakabal wa taifa hili.

Akizungumza leo Ijumaa katika shule ya msingi ya Athi River, Dkt. Omollo alisistiza haja ya kuwalinda wanafunzi dhidi ya kuacha shule na utumizi wa dawa za kulevya.

“Watoto wetu ni rasimali muhimu. Hatuwezi wapoteza kupitia mihadarati, uhalifu au kukosa matumaini. Wazazi wamewekeza pakubwa kuhakikisha wanao wanapata elimu. Kama serikali tumejitolea kuhakikisha kila mtoto haendi shule tu, lakini pia analindwa dhidi ya madhara yoyote,” alisema Dkt. Omollo.

Katibu huo alitoa wito kwa maafisa wa serikali ya taifa kushirikiana kwa karibu na viongozi wa shule, vyama vya wazazi na makundi ya kidini kuhakikisha wanafunzi wanahudhuria masomo, akisema kuwa wizara yake itaimarisha usaidizi wake.

Aidha alikashifu ongezeko la visa vya utumizi wa mihadarati hasaa katika mitaa iliyo karibu na barabara kuu kama vile Athi River, akiwaonya walanguzi kuwa watachukuliwa hatua kali.

Dkt. Omollo aliyasema hayo alipoongoza machifu katika upanzi wa miti chini ya mpango uliozinduliwa mwaka 2024 wa Chief’s Climate Action Day, ambayo huadhimishwa kila mwezi kote nchini.

Mpango huo unalenga kuhakikisha machifu wanafanikisha lengo la serikali la upanzi wa miti bilioni 15 kufikia mwaka 2032.

Hafla hiyo iliwaleta pamoja viongozi wa shule ya msingi ya Athi RiverMachifu na Manaibu wao, wawakilishi kutoka NACADA na maafisa wengine wa serikali.

Website |  + posts
Share This Article