Dkt. Kipsang, Makatibu wengine 5 wahamishiwa Wizara zingine

Martin Mwanje
1 Min Read
Dkt. Belio Kipsang - Katibu wa Elimu ya Msingi anayeondoka

Jumla ya Makatibu 6 wamehamishiwa Wizara zingine katika mabadiliko ya hivi punde yaliyofanywa na Rais William Ruto katika serikali yake.

Katika mabadiliko hayo, Dkt. Belio Kipsang amehamishwa kutoka Wizara ya Elimu na kuteuliwa kuwa Katibu wa Idara ya Uhamiaji na Huduma za Raia katika Wizara ya Usalama wa Taifa.

Idara hiyo awali ilishikiliwa na Prof. Julius Bitok ambaye sasa ameteuliwa kumrithi Dkt. Kipsang kama Katibu wa Idara ya Elimu ya Msingi.

Teresiah Mbaika amehamishwa kutoka Wizara ya Ugatuzi na kuteuliwa kuwa Katibu wa Idara ya Usafiri wa Anga katika Wizara ya Barabara na Uchukuzi wakati Harry Kimtai akihamishiwa Wizara ya Madini.

Kimtai anarithi nafasi ya Elijah Mwangi ambaye ameteuliwa kuwa Katibu katika Wizara ya Michezo.

Naye Mwangi anachukua mahali pa Peter Tum ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Kenya katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Ismael Madey ameteuliwa kuwa Katibu wa Idara ya Mipango Maalum katika Wizara ya Utumishi wa Umma.

Awali, Madey alihudumu kama Katibu wa Idara ya Masuala ya Vijana na Uchumi Bunifu.

Website |  + posts
Share This Article