Andry Rajoelina amehifadhi kiti cha urais nchini Madagascar baada ya kuzoa zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa.
Kwenye matokeo yaliyotangazwa juzi Jumamosi na tume huru ya uchaguzi nchini humo, Rajoelina ambaye zamani alikuwa DJ alipata asilimia 58.95 ya kura zote zilizopigwa.
Rajoelina atahudumu kwa kipindi kingine cha miaka mitano baada ya kuwabwaga wapinzani wengine 12 katika raundi ya kwanza ya upigaji kura.