Dickson Ndiema aliyemchoma moto Rebecca Cheptegei amefariki

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei

Dickson Ndiema anayedaiwa kumchoma moto mwanariadha raia wa Uganda Rebecca Cheptegei, amefariki.

Ndiema alifariki alipokuwa akitibiwa majeraha ya moto katika hospitali ya mafunzo na rufaa ya Moi Jijini Eldoret.

Hospitali hiyo ilithibitisha kuwa Ndiema alifariki akipokea matibabu katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU.

Ndiema anadaiwa kumvamia Cheptegei kwa kumwagilia mafuta ya petroli na kumchoma moto, ambapo madaktari walisema mwanariadha huyo alichomeka asilimia 80.

Katika kisa hicho, Ndiema pia alipata majeraha ya moto, baada ya mwili wake kuchomeka asilimia 30.

Wawili hao walikuwa wamelazwa katika hospitali ya mafunzo na rufaa ya Moi, Eldoret.

Rebecca atazikwa kwa kuzingatia sherehe za kijeshi, kwani alikuwa mwanajeshi wa UPDF.

Share This Article