DCI yatangaza kuzima kabisa biashara haramu ya bidhaa za Petroli

Tom Mathinji
1 Min Read

Idara ya polisi wa uchunguzi kuhusu maswala ya jinai DCI, imetangaza kushinda vita dhidi ya biashara haramu ya bidhaa za petroli katika barabara ya Kisumu – Busia.

Kupitia mtandao wa X, idara hiyo ilisema eneo la Sindindi ambalo lilikuwa maarufu kwa biashara haramu ya mafuta, sasa ni mahame kufuatia operesheni ya maafisa hao wa DCI.

DCI ilisema ilianzisha operesheni ya kitaifa dhidi ya walanguzi wa bidhaa za petroli ambao hufyonza mafuta kutoka kwa malori ya masafa maferu, na kuuza mafuta hayo kwa bei ya rejereja.

Kulingana na idara hiyo, biashara hiyo haramu ni hatari sana na wakati mwingine husababisha kuzuka kwa moto.

“Msako wa kitaifa ulizinduliwa kukabiliana na biashara haramu ya uuzaji na usambazaji wa mafuta ambayo imesababisha kuzuka kwa moto,” ilisema idara ya DCI kupitia mtandao wa X leo Jumamosi.

Idara hiyo ilitoa wito kwa wanaotekeleza biashara hiyo haramu, kujihusisha na biashara halali, ikizingatiwa hatari inayozingira biashara haramu ya mafuta.

Ilisema msako huo ungali unaendelea.

TAGGED:
Share This Article