DCI yamtaka Gachagua kaundikisha taarifa kwa madai ya kuawa

Dismas Otuke
1 Min Read
Rigathi Gachagua.

Idara ya uchunguzi wa kesi za jinai imemtaka aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, kuandiskisha taarifa kesho Oktoba 22, kuhusiana na madai ya majaribio mawili ya kuawa na maafisa  huduma ya kitaifa ya ujasusi NIS.

Kwenye hotuba yake Jumapili baada ya kutoka kwenye hospitali ya Karen,Gachagua ambaye aliyeng’olewa mamlakani na bunge la Senate,alidai kuwa maafisa wa NIS walijaribu kumtilia sumu akiwa kaunti ya Kisumu Agosti 3,0 na baadaye Septemba 3 akiwa kaktika kaunti ya Nyeri akiwa na wazee wa jamii ya Kikuyu.

Jaji Mkuu Martha Koome anatarajiwa kutoa mwelekeo jinsi kesi iliyowasilishwa na mawakili wa Gachagua kupinga kutimuliwa kwake ofisini itavyosikizwa.

Makahama kuu isilistisha uapisho wa mrithi wa Gachagua ,Kithure Kindiki aliyeidhinishwa na bunge kuwa Naibu mpya wa Rais, hadi pale kesi hiyo itakapoamuliwa.

Share This Article