DCI kushirikiana na Safaricom kukabiliana na ulaghai

Tom Mathinji
1 Min Read

Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI imejitolea kuimarisha ushirikiano wake na kampuni ya huduma ya mawasiliano ya rununu ya safaricom.

Mkurugenzi wa idara hiyo Mohamed Amin amesema ushirikiano huo utajumuisha uchunguzi wa visa vya ulaghai vinavyotekelezwa kupitia mtandao wa kampuni hiyo.

Amin aliyasema hayo alipowapokea maafisa wa ngazi za juu wa kampuni ya Safaricom waliomtembelea katika makao makuu ya idara hiyo jana Jumatano.

Aliuhakikishia ujumbe huo ulioongozwa na James Kiama kujitolea kwa DCI kushirikiana na kampuni hiyo kwani inawahudumia mamilioni ya Wakenya.

Amin alibaini kwamba wahalifu wenye ujuzi wa teknolojia wamechukua fursa ya ukuaji wa haraka wa teknolojia kuendeleza shughuli za uhalifu.

Aidha alisema ni sharti kuwepo mabadiliko ya mkakati kati ya kampuni za huduma za mawasiliano na vyombo vya usalama.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *