Mwanamuziki wa mtindo wa “Afrobeat” David Adeleke, maarufu kama Davido atafanya harusi ya kitamaduni kesho Jumanne, Juni 25, 2024 jijini Lagos nchini Nigeria.
Davido atakuwa anahalalisha ndoa yake na mpenzi wake Chioma Rowland na alichapisha picha za kabla ya harusi hiyo ya kitamaduni kwenye mitandao ya kijamii.
Wiki iliyopita Davido alithibitisha ujio wa harusi hiyo.
Davido na Chioma wamekuwa wapenzi kwa muda mrefu ingawa Davido ana watoto na wanawake wengine. Mwisho wa mwezi Oktoba mwaka 2022, wawili hao walifiwa na mwanao wa kiume ambaye alizama kwenye kidimbwi cha kuogelea nyumbani kwao.
Kabla ya mazishi ya mtoto huyo, Davido na Chioma walifanya matambiko ya kitamaduni ya kuashiria kwamba wao ni wanandoa ili kuruhusu maziko ya mtoto huyo kwa jina Ifeanyi Adeleke Jr.
Kulingana na ripoti wawili hao walijaliwa watoto mapacha.