David Mugonyi ateuliwa Mkurugenzi Mkuu wa Halmashauri ya Mawasiliano

Tom Mathinji
1 Min Read

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya rais, David Mugonyi ameteuliwa kuwa mkurugenzi mkuu mpya wa halmashauri ya mawasiliano humu nchini, CA.

Uteuzi wa Mugonyi umejiri baada ya mahojiano ya kujaza nafasi hiyo yaliofanywa mwezi Novemba.

Akitangaza uteuzi huo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali Eliud Owalo aliagiza bodi ya halmashauri hiyo kurasimisha uteuzi huo.

Mugonyi anachukua mahali pa Ezra Chiloba aliyesimamishwa kazi mwezi Septemba, kwa madai ua utumizi mbaya wa mamlaka na fedha za mpango wa rehani wa ununuzi wa nyumba za wafanyakazi.

Baadaye, Chiloba alijiuzulu kutoka wadhifa huo.

Share This Article