Croatia yawagutusha wenyeji Uholanzi na kuingia fainali UEFA Nations League

Dismas Otuke
1 Min Read

Croatia waliigutusha Uholanzi mbele ya mashabiki wa nyumbani kwa kuwatitiga magoli 4-2, kupitia muda wa nyongeza kufuatia sare ya 2-2 katika nusu fainali ya kwanza Jumatano usiku mjini Amsterderm.

Donyell Malen aliwaweka wenyeji kifua mbele kunako kipindi cha kwanza dakika ya 34, kabla ya Andrej Kramaric kuwarejesha wageni mchezoni mwanzoni kipindi cha pili kupitia mkwaju wa penati.

Hata hivyo utepetevu wa safu ya ulinzi ya Croatia kulimruhusu Noa Lang, kutikisa nyavu kunako dakika ya 96 na kubidi mshindi abainishwe kupitia dakika 30 za ziada.

Mzee wa kazi Luka Modric, alipachika goli moja na kuchangia jingine katika muda wa mazidadi .

Croatia watakutana na mshindi wa semi fainali ya pili Alhamisi usiku, kati ya Uhispania na Italia katika fainali ya Jumapili .

Itakuwa fainali ya pili kuu kwa Croatia tangu wapoteze fainali ya kombe la dunia mwaka 2018 dhidi ya Ufaransa.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *