Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi nchini Kenya, COTU umeipongeza serikali kupitia kwa Wizara ya Leba kwa kutekeleza nyongeza ya mshahara kwa asimili 12, kama alivyotangaza Rais William Ruto wakati wa sherehe za Leba Dei mwaka huu.
Wizara ya Leba imechapisha kenye gazeti rasmi la serikali nyongeza ya mshahara wa chini kwa asilimia 12 na asilimia 15 kwa wafanyakazi wa sekta za kilimo.
Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli amesema utekelezwaji wa nyongeza hizo zilizotagazwa mjini Vihiga mwezi jana, ni ishara ya serikali kuwajali wafanyakazi wa chini.
Atwoli ameitaka Wizara ya Leba kufanya ukaguzi kuhakikisha agizo hilo linazingatiwa na waajiri wote.