Timu ya Urugua imewabandua mabingwa mara tisa Brazil mapema hii leo kwenye mashindano ya Copa Amerika yanayoendelea nchini Marekani kupitia matuta ya 4-2 baada ya sare ya yai katika muda wa kawaida.
Kati ya mechi saba walizocheza katika siku za hivi karibuni, Brazil na imeshinda mara nne, sare moja, nayo Uruguay imeshinda mara mbili.
Kufuatia ushindi huo, Uruguay itakabana koo na Colombia kwa nusu fainali tarehe 11 saa tisa usiku.